Wednesday, July 13, 2016

UWE NAMI BWANA lyrics by Solomon Mukubwa

Eh Bwana umeniita nikutumikie
kwenye kizazi hiki kimejaa matatizo
Usiponishika mkono Bwana
nani mwingine atanishika
ninachokuomba Baba, Uwe nami
Umeniita jinsi nilivyo
nimebeba msalaba wangu
sijali majaribu, nimekuja Kwako
nisaidie nijipe moyo
ili nifikirie taji
ninachokuomba Baba, Uwe nami
matatizo yamejaa kwote
wanadamu wamechoka, wengine wamekuacha
tupe neno tuwaendee nawapate Kukujua
ninacho kuomba Baba, Uwe nami

  (CHORUS)
Yesu, Uwe nami, ona watumishi wako Baba
Yesu usiniache
dunia shida nyingi, matatizo yasumbua moyo
ninachokuomba Baba, Uwe nami
Yesu, Uwe nami, mlima ni mrefu sitaweza
Yesu usiniache
dunia shida nyingi, matatizo yasumbua moyo
ninachokuomba Baba, Uwe nami

Wako wengi wamejeruhiwa
waite wakusajili
Usiwapite Bwana, Jionyeshe kuwa Wewe Baba
Usiwaache waangamie, shetani amefungua kinywa kuwameza
ninachokuomba Baba, Uwe nao
wengine wameshindwa kwenye ndoa zao
wameamua kuachana, Bwana nakuomba uwaone
matatizo yamewacha, bila Wewe wataachana
ninakuomba Uwe nao
matatizo ya huduma yamejaa
Usiposimamaisha watumishi Wako Baba
nani atawasimamisha
shetani ametega mitego, Eh Bwana Tusaidie
tufike mwisho wa safari yetu tupate taji
Uwe nasi

  (CHORUS)
Yesu, Uwe nami, ona watumishi wako Baba
Yesu usiniache
dunia shida nyingi, matatizo yasumbua moyo
ninachokuomba Baba, Uwe nami
Yesu, Uwe nami, mlima ni mrefu sitaweza
Yesu usiniache
dunia shida nyingi, matatizo yasumbua moyo
ninachokuomba Baba, Uwe nami

Uwe nami, Uwe nami, Uwe nami
Usiniache
Uwe nami, Uwe nami
nachokuomba Baba, Uwe nami
Usiniache
Uwe nami, Uwe nami, Uwe nami
Usiniache
Uwe nami, Uwe nami, Uwe nami
Usiniache
Uwe nami, Uwe nami, Uwe nami
Usiniache

No comments:

Post a Comment