Wednesday, July 13, 2016

KAMA SIO WEWE lyrics by Mercy Wairegi ft Billy Frank

(Mercy Wairegi)
pendo gani hili
bwana ukanipenda
kabla nikujue
wewe umenipenda
mimi nani sasa
bila wewe maishani
kabla nikujue
wewe ulinipenda
na wakati nakukosea
Bwana wee wanisamehe
waniita mwana wako
hata wakati ni dhaifu
sistahili mbele zako
naja kwa unyenyekevu
kwani mimi bila wewe
mimi si kitu, si kitu

  (CHORUS)
ningekuwa wapi
kama si wewe
ningeitwa nani
kama si wewe
ningefanya nini
kama si wewe
kwani bila wewe
mimi si kitu

  (Billy Frank)
nikikumbuka jinsi ulivyo
sina la kusema
nilipotea
kwenye dhambi ukaniokoa
mimi ni nani
mbele zako
kama sio wewe
ningekuwa wapi
kama si wewe
ulinipenda
ukanionyesha njia
ulinipenda
ukaniokoa sina mwingine

  (CHORUS)
ningekuwa wapi
kama si wewe
ningeitwa nani
kama si wewe
ningefanya nini
kama si wewe
kwani bila wewe
mimi si kitu

(Mercy Wairegi)
najitoa kwako bwana
uinuke ndani yangu
mimi kwako mtumishi
nitumie upendavyo
najitoa kwako bwana
nitumie upendavyo
mimi kwako mtumishi
nakuomba nitumie
nijaze, nijaze
nijaze na roho yako
nifinyange, nitumie, najitoa mbele zako

  (CHORUS)
ningekuwa wapi
kama si wewe
ningeitwa nani
kama si wewe
ningefanya nini
kama si wewe
kwani bila wewe
mimi si kitu

1 comment:

  1. Thanks for the lyrics, Uploaded to http://sifalyrics.com/kuabudu the main worship directory

    ReplyDelete