Wednesday, July 13, 2016

KAMA NITAKUFA LEO lyrics by Solomon Mukubwa

Nimeona urafiki wa dunia
si kama urafiki wangu na Yesu
hapa duniani, bibi yako akifariki Baba
upendo wenu utaishia makaburini
nimeona urafiki wa dunia
si kama urafiki wangu na Yesu
mume wako akifariki Baba
upendo wenu utaishia makaburini
Nimeona urafiki wa dunia
si kama urafiki wangu na Yesu
rafiki yangu ukifa leo, sisi na jamaa lako
upendo wetu mwisho ni makaburini
Nimeona urafiki wa dunia
si kama urafiki wangu na Daddy Yesu
Anasema mimi nikifa, Atanifufua hadi binguni
nitanyakuliwa naye tuingie binguni

  (CHORUS)
Sijaona rafiki kama Yesu...
ata nikifa, atanifufua kwenda binguni
sijaona rafiki kama Yesu
Sijaona rafiki kama Yesu...
ata nikifa, atanifufua kwenda binguni
sijaona rafiki kama Yesu

Usilie wewe uliachwa
watoto msilie mliachwa na wazazi
mtetezi wenu Yuko juu Anaona
mbona wawatesa hawa yatima waliobaki na wewe?
wawatendea vibaya
mtetezi wa yatima, baba yao yuko juu
Atajibu kwa wakati wowote
ni rafiki, ni rafiki, Hamkatai mtu
Anatupenda wote sawa
daddy hakuna kama wewe
baba na mama wanaweza kukuwacha ndugu
marafiki wanaweza kukutoroka
sijaona rafiki kama wewe, Utakaye nifufua

  (CHORUS)
Sijaona rafiki kama Yesu...
ata nikifa, atanifufua kwenda binguni
sijaona rafiki kama Yesu
Sijaona rafiki kama Yesu...
ata nikifa, atanifufua kwenda binguni
sijaona rafiki kama Yesu

Urafiki wa dunia si kama wa Yesu ooh
marafiki wa dunia wanaachana njiani
lakini Yesu ukichoka, anakupeleka hadi mwisho wako ndugu
marafiki wa duniani wa faida
ukiwa na hela utapata marafiki wengi
lakini wacha zikwishe, wanabaki wanaongea vibaya
alikua amejivuna sasa zimekwisha
marafiki wa dunia si wa faida kama daddy
ukifa wanakuwacha kaburini
Yesu ni rafiki mwema, hawezi kuwacha, wakati wa shida atakuinua

  (CHORUS)
Sijaona rafiki kama Yesu...
ata nikifa, atanifufua kwenda binguni
sijaona rafiki kama Yesu
Sijaona rafiki kama Yesu...
ata nikifa, atanifufua kwenda binguni
sijaona rafiki kama Yesu

No comments:

Post a Comment