Wednesday, January 13, 2016

MAMBO YABADILIKA lyrics by Hellena Ken


Huu, ni mwaka wa urejesho  x2
Mambo, mambo yabadilika x2
(Repeat)

(CHORUS)
Naona mambo yakibadilika
(Yabidilika kwa wema wako)
(REPEAT)

Mambo, mambo yabadilika  x2
Walio chini sasa, naona wakiinuliwa
Walio nyuma sasa, naona wakiwa mbele
Wanaodharauliwa, naona heshima zao
Wanaolia sasa, machozi yanapanguzwa

Huu ni mwaka wa urejesho x2
Uliyepoteza ndoa, naona ikirejeshwa
Uliyepoteza watoto, naona wakirejeshwa
Uliyepoteza nyumba, naona ikirejeshwa
Uliyepoteza kazi, naona ikirejeshwa
Uliyepoteza cheo, naona kikirejeshwa
Uliyepoteza heshima, naona ikirejea
Kwani mambo yabadilika

(CHORUS)

Majina yaenda kubadilika  x2
Wanaoitwa tasa, naona wakiitwa mama
Wanaodharauliwa, naona heshima zao
Wanaoitwa duni, sasa wainuliwa
Walio pekee yao, waenda pata wachumba
Kwani mambo, mambo yabadilika  x2

Wanaolia sasa, machozi wanapanguza
Waliokataliwa, sasa wakubalika
Wasio na makao, wapata makao yao
Wasio na amani, wapata amani yao
Wasio na furaha, wapata furaha yao
Kwani mambo, mambo yabadilika  x2

(CHORUS)

Jipe jina, tutakuita unapojiita sasa 
Pokea jina jipya, maana majina yabadilika

Refrain: Naitwa mbarikiwa
Tukuite nani nani leo
Jipe jina, jipe jine
Na wewe waitwa nani leo
Baba yangu tukuite nani
Jipe jina, jipe jine

(CHORUS)

No comments:

Post a Comment