Tuesday, April 19, 2016

TULIA lyrics by Benachi

Amesema utulie, amesema utulie
Amesema utulie

Mwezangu ninakuona, umekazana sana
Kila kunapokucha, mawazo yamekubana
Maneno umenena, kwenye sala aaah
Umekesha kuomba, fungu la kumi umetoa
Pia kufunga lakini bado
Umekesha kuomba, usichoke kuomba
Mkono wake si mfupi utakufikia

  (CHORUS)
Tulia, hajawai chelewa wakati wake mwema
Tulia, usife moyo kilio amekiskia
Tulia, usichoke kuomba, piga moyo konde
Tulia, imani juu, imani juu, imani kwake
Tulia, imani juu, imani juu, imani kwake

Tazama juu, msaada wako watoka juu
Kutoka chini mola atakuweka juu
Na ushawai jiuliza mbona hausongi juu
Ni kwa sababu muda wako utafika tu
Vumilia tu muda wako utafika tu
Na ukiwadia hakuna ambaye atazuia
Ukitimia aaah aaah, hatazuia

  (CHORUS)

Tazama juu msaada wako watoka juu
Kutoka chini mola atakuweka juu
Na ushawai ooh....

  (CHORUS)

No comments:

Post a Comment