Tuesday, April 19, 2016

TENDA WEMA lyrics by Ringtone ft Christine Shusho

 
(CHORUS)
Tenda wema nenda zako
Usisahau Mungu anaona

Siku ya kukumbukwa itafika

Yeye, yeye, yeye atakulinda
Tenda wema nenda zako
Usisahau Mungu anaona
Siku ya kukumbukwa itafika...

  Ringtone
Mayatima umesomesha sana, kwenye shida umesaidia wote
Wenye njaa umewapa chakula, nguo zako umepeana zote
Hakuna anayetambua haya ambayo umetenda kwote
Sasa naona inakupa worry, nakuomba wee usijali
Aliyekuita anaona yote, atabariki ona siku zote

  (CHORUS)

  Christine
Aliwaponya wagonjwa wao ni yesu huyo
Akafufua wafu wao ni yesu huyo
Mwisho akamwita pepo huyo oooh
Wewe si wa kwanza na hautakuwa wa mwisho
Yesu katukanwa sembuse mwanadamu
Tenda wema nenda zako weee
Usigonje shukurani wee
Tenda wema nenda zako weee
Usigonje shukurani wee

  (CHORUS)

  Ringtone
Utawasomesha wajue kizungu, wakutusi
Utawalisha washibe wakupige
Wewe tenda mema, wewe tenda mema tu
Wewe tenda mema, wewe tenda mema tu

  (CHORUS)

1 comment: