Thursday, January 7, 2016

BADO NASIMAMA Lyrics by Kambua

  (CHORUS)
Bado nasimama, bado naendelea
Bado najikaza nifike kulee ×2

Bila neema na rehema zako, ningekuwa wapi mimi
Bila upendo na fadhili zako, maisha yangu yangekuwa bure
Kwa wema wako kanisimamisha na imani yangu ukaiweka salamaa
Kama si wewe mwamba wa wokovu wangu
Nisingeweza ningeangamia

  (CHORUS)

Nainua macho yangu, kwako ewe baba yangu
Msaada wangu utatoka wapi, msaada wangu u katika bwana
Asinzii, anilindae aniachi mimi nitelezee uuuhh
Anipa nguvu na uwezo wake ili mimi nifike kule
Nifike kuleee....

  (CHORUS)

UWEPO lyrics by Mercylinah Wambungu

  (CHORUS)
Uwepo wako nahitaji maishani
Uwepo wako wa dhamana sana
Mimi sitoki hata siendi bila uwepo wako
Bwanaa, bwanaa ×2

Ninapowezwa na magonjwa (Ninaye Jehovah Rapha)
Nikiwa na mahitaji (Ninaye Jehovah Jireh)
Amani ninapoikosa (Ninaye Jehovah Shalom)
Moyo wangu tulia (Tunaye Jehovah Shamah)
Shauku la moyo wangu nipate zaidi yako
Zaidi na zaidi na zaidi

  (CHORUS)

Hakuna cha kuogopa (Nunaye El Olam)
Mungu muumbaji wangu (Ndiye Elohim)
Mchungaji wangu (Ndiye Jehovah Rohi)
Tena msaidizi wangu (Ndiye Jehovah Elyon)

  (CHORUS)

Katika uwepo wako;
Kuna uponyaji, twawekwa huru, kuna amani tena furaha, kuna ushindi, msamaha, twatiwa nguvu

  (CHORUS)

WEWE PEKEE Lyrics by Alice Kamande

Kufungua kinywa changu, nikusifu baba
Makuu umenitendea, nimefika sasa apa
Wewe kweli ni rafiki, unaniongoza ninapopotea
Upendo wako ni ufananishe na nani babaa

  (CHORUS)
Tabu nyingi kweli nlipitia (hadi nikajipata nikikushukuru)
Sikujua mpango wako kwangu (babaa)
Ulijua yote nikiyapitia mkono wako ulikuwa umenishikilia nisianguke ewee wewee kimbilio langu
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako
Mbele ata nyuma, ni wewe pekee ×2

Tafuta tafuta utampata kama yeye alinitoa toka tope la dhambi
Kamwe sitaona aya ya kumsifu mungu wangu

  (CHORUS)

Monday, January 4, 2016

NIKUPENDEZE

Mienedo yangu na tabia zangu zikupendeze
Kuvaa kwangu na kunena kwangu kukupendeze ×2
Nifanane na wewe yesu
Niwe jinsi upendavyo
Niguze nifinyange, unibebe
Niunde nitengeneze, niwe kama wewe

  (CHORUS)
#Nikupendeze, Nikupendeze

Familia yangu, marafiki zangu tuwe sawa na wewe
Biashara zangu, kila kitu changu kiwe sawa na wee ×2
Niguze nifinyange unibebee
Niunde nitengeneze niwe kama wewe

  (CHORUS)

Nifanane na wewe yesu
Niwe jinsi upendavyo
Niguze nifinyange unibebe
Niunde nitengeneze niwe kama wewe

  (CHORUS)

ULIBEBA Lyrics by Eunice Njeri

  (CHORUS)
Uliibeba yote, uliibeba yote
Ulisema yote yamekwisha
Ulibeba yote

Ulidharauliwa na kukataliwa
Mtu wa huzuni mingi, aijuaye mateso
Wanadamu tulikufichia uso, kukuona bure
Ata hivo udhaifu wetu, uzuni zetu ulichukua yesu
Mijeledi kuchipuliwa na makosa maovu yetu
Adhabu kubwa ili sisi tupate amani
Kwa majeraha yesu sote tumepona
Asante yesu kwa neema na wokovu wako

  (CHORUS)

Kuwa nao na ata kuteswa bila wewe yesu
Hukusema chochote baba
Kuongozwa kama kondoo kwenye kichinjio
Ulinyamaza kimia baba ata hivo kukataliwa na wote walio uhai
Kufanyiwa kaburi yesu pamoja na waovu
Mapenzi yake bwana kuwa wewe uteseke maisha yako yesu sadaka ya hatia yangu eeeh

  (CHORUS)

Uliamini na maisha yako, hadi mauti kuhesabiwa pamoja nasisi wakosaji dhambi za wengi ulizichukua, kutuombea sisi wenye makosa
Ingawa usawa na mungu, kukuona kama kitu
Chakushika na macho ni sawa na mtumwa kunyenyekea hadi mauti
Mauti ya msalaba kuokoa mataifa yote eeeh

  (CHORUS)

Ona sasa mimi nashukuru, nafurahia
Sina deni mie, sasa niko huru
Hakuna deni tena yesu ashalipa

UNATOSHA Lyrics by Eunice Njeri

Nimeubeba msalaba wangu, nikufuate wewe uliyenipenda
Nimeitua mizingo yangu kwako, nakufwata wewe unayenipenda ×2

  (CHORUS)
Bwana unatosha
Wanitoshaa... mungu wa agano
Wewe wanitosha ×2

Nasalimu amri yako eeeh baba
Sauti yako nimeisikia
Umenivuta bwana karibu na wewe
Karibu zaidi natamani niwe ×2

  (CHORUS)

Moyo wangu usawa sioni ovu
Wanitosheleza wanitosha...
Mwingine mie sina, wewe wanitosha
Wanitoshaaa wanitoshaa...

  (CHORUS)

NIACHE NIIMBE Lyrics by pitson

Siku moja mama nitakujengea nyumba ya kifahari
Uishi poa mama na pesa za mziki
Siku moja baba nitakununulia gari la kifahari
Uendeshe baba na mziki
Siku moja dada nitakulipia karo ya shule
Uende university na pesa za mziki
Siku moja brother nitakufungulia biashara kubwa
Uwe sonko brother na pesa za mziki

  (CHORUS)
Ikiwa nitakuwa rubani, niendeshe ndege
Niwe rubani, rubani anaimba
Ikiwa nitakuwa karani, karani wa benki
Niwe karani, karani anaimba
Ikiwa nitakuwa waziri, waziri wa serikali
Niwe waziri, waziri anaimba
Oooh popote niendapo, chochote nifanyacho
Yeyote nitakuwa niwe naimba
Mama na baba naomba mniache niimbe
    #Niache niimbe
Shule nitaenda lakini mniache niimbe
Kazi nitafanya lakini mniache niimbe
Mimi naahidi kuwa nitaimba nyimbo za injili

Mungu ni mwaminifu ×4
Hakuna anaweza sema hajapewa kitu cha kufanya
Mungu ni mwaminifu
Wengine wanauza nguo gikosh
Wengine wanashona, wengine wamekonda wanakimbia
Ma-bouncer wameshona
Wengine ma odijo -polisi -CEO-
Ma hustler

  (CHORUS)